Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza mradi wa machinjio ya kuku katika mji wa Karbala, yenye uwezo wa kuchinja hadi kuku (5000) kwa saa.

Maoni katika picha
Machinjio ya Karbala imeanza kuzalisha nyama baada ya kuifanyia matengenezo na kuiboresha, kwani ilisimama kufanya kazi kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na saba, na kurudisha uhai upya kwenye kiwanda hicho muhimu hapa mkoani kinacho changia uchumi wa taifa.

Machinjio hiyo aliwashwa siku za nyumba kwa ajili ya majaribio na baada ya kufanya kazi vizuri ndio imewashwa moja kwa moja, inafanya kwazi kwa kiwango ilicho pangiwa na inaweza kuchinja hadi kuku (5000) kwa saa siku za mbele, uwezo huo ilikua haina siku za nyuma.

Mhandisi Muhammad Ashiqar katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ametembelea machinjio hiyo akiwa na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi pamoja na marais wa vitenge vya Ataba, kuangalia utendaji wa machinjio hiyo, na akauambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Miongoni mwa mitazamo na malengo ya Atabatu Abbasiyya ni kufanya kila kinachosaidia taifa kujitegemea, machinjio hii ni moja ya miradi mingi inayo kusudia kufikia lengo hilo, watumishi wetu wameifanyia matengenezo machinjio hii iliyojengwa katika miaka ya themanini karne iliyopita na ikasimama kufanya kazi tangu mwaka 2003, na kutelekezwa hadi vifaa vingi vikaharibika kabisa, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu imeanza kufanya kazi upya kwa kiwango kikubwa zaidi ya ilivyo kuwa miaka ya nyuma, itachangia pato la taifa na kuhamasisha ufugaji wa kuku hapa nchini, machinjio hii itasaidia kutoa ajira kwa wananchi na kuhakikisha upatikanaji wa kipato cha uhakika kwa wafugaji wa kuku, mambo yote hayo yanachangia pato la taifa”.

Mwenyekiti mtendaji wa shirika la Liwaaul-Aalamiyya Mhandisi Aadil Maliki Muamaar shirika lililofanya matengenezo ya machinjio hiyo na kusimamia utendaji wake amesema kuwa: “Kazi ya matengenezo imefanyika kwa muda wa mwaka mmoja na nusu takriban, tumetengeneza sehemu za kuchinjia kwa kurekebisha na kununua mitambo mipya itakayo wezesha kupokea kiwango kikubwa cha kuku na kuwachinja kwa njia ya kisasa kwenye mazingira mazuri, sambamba na kujenga mtambo wa kusambaza maji, kuweka mfumo mzuri wa umeme, sehemu ya vyoo, kamera za ulinzi na mfumo wa kutoa tahadhari, zima moto pamoja na mambo mengine mengi, yote hayo yameiwezesha machinjio hii kufanya kazi kisasa na kwa kiwango kikubwa kinacho endana na ongezeko la kuku, hadi kufikia uwezo wa kuchinja kuku (5000) kwa saa”.

Shekh Swalahu Khafaji rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu amefafanua kuhusu namna ya uchinjaji, amesema: “Tunachinja kwa mujibu wa sheria za kiislamu chini ya usimamizi wa watumishi wa kituo cha kiislamu Alkafeel kilicho chini ya kitengo chetu, kinauzowefu wa kazi hii kwa zaidi ya miaka kumi, tunao wataalam waliobobea na wajuzi wa mambo ya kisheria na kiafya”.

Kumbuka kuwa shirika la Nurul-Kafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limesaini mkataba na shirika ya Karbala wa kuingiza nyama za kuku, kwa lengo la kukarabati na kuanza kufanya kazi upya machinjio ya Karbala iliyopo barabara ya (Karbala – Baabil) kitongoji cha Ibrahimiyya, mradi huu unalenga kuongeza pato la taifa na kuingiza nyama za kuku katika soko la Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: