Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kazi ya kusafisha moja ya malango ya Karbala

Maoni katika picha
Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kazi ya kusafisha moja ya malango ya mkoa wa Karbala kutokea Najafu Ashrafu, kazi hiyo inahusisha eneo kubwa pamoja na upande wa lango la (Baabil – Karbala) na (Bagdad – Karbala) pamoja na ukanda wa kijani uliopo pembezoni mwa mpaka wa mkoa.

Makamo rais wa kitengo tajwa Ustadh Muhammad Harbi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi hii ni muendelezo wa kazi zilizo tangulia, kwa ajili ya kuhakikisha mji unakuwa katika muonekano mzuri, ukizingatia kuwa usafi ni jukumu la wote, na maeneo hayo yanaakisi picha ya mji, kwa hiyo yanatakiwa kuwa safi, na hii ndio kazi tunayo fanya”.

Akaongeza kuwa: “Tumeweka mkakati wa kuondoa taka zote, tumeteua kundi maalum la kufanya kazi hiyo, pamoja na jopo la wataalamu, kazi hiyo inahusisha kusafisha barabara zinazo elekea Karbala pamoja na njia ya (Yaa Hussein) inayo tumiwa na mazuwaru wengi”.

Akamaliza maelezo yake kwa kutoa wito kwa kila anayekuja katika mji huu mtakatifu azingatie usafi, kwa ushirikiano wenu tutaweza kumaliza tatizo hili, hakika usafi ni kitu kizuri, njia ni mali ya kila mtu hivyo yapasa wote tushirikiane kudumisha usafi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: