Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya ametembelea shule ya msingi Nurul-Ameed ya wavulana

Maoni katika picha
Mheshimiwa kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea shule ya msingi Nurul-Ameed ya wavulana, ziara hii ni sehemu ya ufuatiliaji wa baba kwa familia yake katika taasisi za malezi na elimu zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ametembelea madarasa ya shule na kuangalia kazi zinazofanywa na idara ya shule pamoja na watumishi wake, ili kutimiza malengo ya shule za Al-Ameed yatokanayo na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuandaa kizazi chenye kujitambua.

Tambua kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inaipa kipaombele sekta ya malezi na elimu, imekua ikitaka kuona mafanikio daima katika taasisi za malezi na elimu, kwa sababu ndio msingi mkuu katika maendeleo ya jamii kidini, kijamii na kitamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: