Maahadi ya Quráni tukufu inafanya semina ya kuhakiki usomaji wa kiiraq na kimisri

Maoni katika picha
Idara ya usomaji wa Quráni na kuandaa wasomi chini ya Maahadi ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa semina ya kuhakiki njia za usomaji wa kiiraq na kimisri, na wameshiriki watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na wanafunzi wa Maahadi katika mji mtukufu wa Karbala.

Semina hizo zimehusisha masomo ya hukumu za tajwidi, sauti na naghma ya Quráni kwa mahadhi ya kiiraq na kimisri, chini ya usimamizi wa Ustadh Alaau-Dini Hamudi Alhamiri na Sayyid Haidari Jalukhani, zaidi ya wanafunzi (40) wameshiriki katika semina hiyo.

Washiriki wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na Maahadi ya Quráni pamoja na walimu wao, kutokana na kazi kubwa wanayo fanya kwenye sekta ya Quráni.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu ni moja ya sehemu muhimu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inayo lenga kueneza elimu ya Quráni tukufu na kuandaa kizazi kinacho fuata mafundisho ya Quráni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: