Zaidi ya maukibu (70) hutoa huduma kwa mazuwaru kila ufikapo usiku wa kuamkia Ijumaa ya kila wiki

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadhu Ni’mah Salmaan amesema kuwa: “Zaidi ya maukibu (70) za kutoa huduma kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, zimekua zikitoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi kila wiki katika usiku wa kuamkia Ijumaa ambao huwa na mazuwaru wengi, mawakibu hizo hukaa kwenye barabara kuu zinazo elekea katika malalo hizo takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Asilimia kubwa ya mawakibu hizo zinatoka nje ya mkoa, na hugawa chakula na vinywaji (maji na juisi), kitengo kimeweka utaratimu maalum katika utoaji wa huduma za mawakibu, kwanza imepangwa idadi maalum kwa ajili ya kuondoa msongamano, hivyo mawakibu zimepangwa kwa makundi, kila kindi linatoa huduma katika wiki maalum, na kundi linalo fuata linatoa wiki nyingine, na kuna kundi ambalo hushiriki kwenye matukio ambayo hushuhudiwa katika mji wa Karbala”.

Akabainisha kuwa: “Kuna mawakibu nyingi na vikundi vya Husseiniyya vilivyo omba kuja kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) katika usiku wa Ijumaa, lakini kitengo kimekataa kwa ajili ya kuzuwia msongamano, mawakibu zilizopo kwa sasa zinatosha na zinatoa huduma zote zinazo hitajiwa na mazuwaru, tumeunda kamati ya pamoja kati ya kitengo chetu na kile kinacho hudumia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu pamoja na askari wanaolinda haram mbili takatifu, kwa ajili ya kuratibu na kusimamia utoaji wa huduma, sambamba na masharti ya kiulinzi na kiafya yaliyo wekwa”.

Akasema kuwa: “Hakika mawakibu zilikua zinatoa huduma katika uwanja wa katikati ya haram mbili miaka ya nyuma, lakini kutokana na msongamano uliokuwa unapatikana hususan katika usiku wa Ijumaa, tukaamua huduma za mawakibu zitolewe nje ya uwanja huo, kwenye barabara zinazo elekea katika Haram mbili takatifu, ikiwemo barabara ya Mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akafafanua kuwa: “Mawakibu zote za kutoa huduma zinazingatia manuni za afya, pamoja na kanuni ya kuandika jina la maukibu, kiongozi na namba yake ya simu, jambo hilo ni muhimu kinidhamu na kiusalama”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: