Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kongamano la Imamu Baaqir (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo mwezi (1 Rajabu 1442h) sawa na tarehe (14 Februali 2021m) imeanza awamu ya saba ya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir (a.s) kilele cha utakatifu na haki ishindayo).

Kongamano lilikuwa na idadi maalum ya washiriki walio hudhuria ukumbini kutokana na janga la Korona, limefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hussein (a.s) na kuhudhuriwa na viongozi wa Dini na sekula kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.

Kongamano limefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na Salim Ammaar Alhilliy, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, akabainisha kuwa: “Ni jambo zuri Atabatu Abbasiyya kufanya kongamano hili kila mwaka na kunufaika nalo kwa kuchota elimu yake na kubainisha utukufu wake na nafasi yake, hilo ndio lengo kuu la Ataba tukufu hata katika awamu ya kongamano la kwanza, kulikua na shindano la muandishi bora kuhusu Imamu Baaqir (a.s), vitabu vilivyo shinda vikachapishwa, kisha awamu ya pili ikawa na utafuti wa mafundisho yake, zikaandikwa mada nyingi na wasomi wa hauza pamoja na sekula…”.

Halafu ukafuata ujumbe kutoka kwa wageni wa kongamano ulio wasilishwa na mwalimu wa hauza katika mji wa Najafu Sayyid Muhammad Ali Bahrul-Uluum, amesisitiza kuwa: “Watu wa Iraq waliwapenda Maimamu wa Ahlulbait (a.s) mapenzi makubwa sana, huo ulikua ndio mtihani wao na alama yao, toka Imamu Ali (a.s) alipoingia Kufa na kuufanya mji huo kuwa makao makuu yake hadi leo, Insha-Allah Iraq wataendelea kuwapenda na kuwaenzi kwa kuufundisha ulimwengu matukufu yao na mwenendo wao pamoja na mafundisho yao bora ya kibinaadamu, yaliyo enea duniani kupitia watoto wao wema walio jitolea kwa hali na mali kusimamisha bendera ya Ahlulbait (a.s)…).

Halafu ikafuata kaswida kutoka kwa mshairi Najahu Arsani, beti zake zimeelezea tukio hili takatifu, kisha ukafunguliwa mlango wa kuwasilisha mada za kitafiti chini ya usimamizi wa Dokta Ali Kadhim Maslawi, na ilikua kama ifuatavyo:

Mzungumzaji wa kwanza: Dokta Jaabir Fariji, mada yake inasema/ Nafasi ya Imamu Baaqir (a.s) katika kuasisi ijtihadi ya Fiqhi.

Mzungumzaji wa pili: Shekh Muhammad Ridhwa Daksan, mada yake inasema/ upotoshaji wa kifikra na nafasi ya Imamu Baaqir (a.s) katika kusahihisha.

Mzungumzaji wa tatu: Dokta Amal Abdujabbaar Sharí kutoka chuo kikuu cha Baabil, mada yake inasema/ Athari ya Imamu Baaqir (a.s) katika kutunza maarifa ya umma wa kiislamu.

Mzungumzaji wa nne: Dokta Numaas Almadani kutoka chuo kikuu cha Karbala, mada yake inasema/ Khutuba za Imamu Baaqir (a.s) katika nadhariya ya akili na mawasiliano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: