Kituo cha turathi za Basra kinafanya nadwa yenye anuani isemayo: (miongoni mwa vinara wa uhakiki katika mji wa Basra)

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibanaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya nadwa yenye anuani isemayo (miongoni mwa vinara wa uhakiki katika mji wa Basra: Dkt. Muhammad Jabbaar – Dkt. Abdulhussein Mubaarak – Ustadh Shaakir Aáshuri kama mfano).

Mhadhiri wa nadwa hiyo alikua Dokta Saami Ali Mansuri, ambaye ameongea kuhusu juhudi za uhakiki za wasomi hao wa Basra, na nafasi yao katika kutunza turathi, akaonyesha umuhimu wa kufanya uhakiki, na changamoto anazo pitia mhakiki, pamoja na kutaja mafanikio ya kielimu ya wanachuoni hao, na sifa maalum ya kila mmoja kati yao, sambamba na kuonyesha uaminifu wa kielimu katika matokeo ya hakiki zao.

Nadwa ilikuwa na maswali mengi pamoja na maoni kutoka kwa washiriki.

Makamo kiongozi mkuu wa idara ya habari Shekh Yasini Yusufu amesema kuwa: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu/ kituo cha turathi za Basra, imechukua jukumu kutunza turathi za mji wa Basra”.

Akafafanua kuwa: “Hakika kituo kinafanya kazi kubwa ya kufuta vumbi kwenye turathi za mji wa Basra, kuzitoa gizani na kuziweka kwenye nuru, ili kuangazia barabara ya elimu ya wanachuoni wa sasa, na leo kupitia nadwa hii tunatoa nafasi kubwa kwa watafiti na wadau wa uhakiki wa turathi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: