Kamati ya maelekezo na msaada imewasili Ainu-Farsi

Maoni katika picha
Kamati ya maelekezo na msaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu imewasili katika kikosi cha kisiwa cha Swalahu-Dini kaskazini kwenye kitongoji cha Ainu-Farsi, kutoa msaada kwa wapiganaji wa Hashdu-Shaábi wanao linda amani katika eneo hilo kutoka kikosi cha sita.

Ziara hii ni muendelezo wa ziara zilizofanywa siku za nyumba na sehemu ya utaratibu iliojiwekea kamati tangu kutolewa kwa fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda, imekua ikisaidia watu walio itikia fatwa hiyo, haijaacha kufanya hivyo wala kudhoofika, bali imeimarika siku baada ya siku, haiwezi kumaliza wiki au mwezi bila kutoka msafara na kwenda kusaidia moja ya vikosi vya wapiganaji.

Rais wa kamati hiyo Shekh Haidari Aaridhwi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumeweka mkakati wa misafara hii ya kusaidia askari wa serikali na wale wa kujitolea (Hashdu-Shaábi), kwa kupanga muda na sehemu kwa kuwapa misaada inayo watia moyo na kuwakumbusha usia wa Marjaa Dini mkuu na kuwahimiza kuuheshimu na kushikamana nao, pamoja na kuwafikishia salamu za watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na dua zao”.

Akaongeza kuwa: “Majemedari hao wamepewa vitu walivyo kuwa wanahitaji kwa sasa, pamoja na baadhi ya zawadi za kutabaruku kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), zinazo watia moyo wapiganaji”.

Kumbuka kuwa tangu ilipo tolewa fatwa tukufu ya kujilinda, kamati hii imekua mstari wa mbele kusaidia vikosi tofauti vya wapiganaji katika vitongoji mbalimbali, misaada hiyo hutolewa moja kwa moja na Atabatu Abbasiyya tukufu au kupitia matawi yake yaliyopo mikoani, kazi hiyo inafanywa karibu kila siku chini ya wasimamizi wa kamati ya ndani au nje ya Ataba.

Wapiganaji wamepongeza juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu, na wameshukuru uwepo wake daima katika uwanja wa vita na katika maeneo yaliyo kombolewa, wakasema kuwa jambo hilo linawatia moyo zaidi wa kuendelea kusimama imara dhidi ya mtu yeyote atakaetaka kuvunja amani na utulivu wa taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: