Wanahabari wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamerusha matukio ya ziara ya Imamu Haadi (a.s) na wameandaa masafa maalum ya bure.

Maoni katika picha
Kikosi cha matangazo ya mubashara chini ya kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel na matangazo ya mubashara kupitia kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa mchango mkubwa katika kurusha matukio ya ziara ya Imamu Haadi (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake jiradi na malalo yake takatifu mjini Samaraa, kwa kushirikiana na wadau wengine katika Atabatu Askariyya takatifu, wamefanikiwa kurusha matukio ya ziara kupitia masafa ya bure ambayo imenufaisha makumi ya vitu vya habari kutoka ndani na nje ya nchi.

Yamesemwa na mkuu wa kituo hicho Ustadh Basiru Taajir, akaongeza kuwa: “Matangazo haya ni sehemu ya mfululizo wa matangazo ya mubashara ndani ya mji wa Samaraa, pia hii ni miongoni mwa ziara zinazo pewa umuhimu mkubwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, hivyo tumeandaa kikosi maalum kinacho fanya kazi ya kurusha matangazo mubashara kupitia masafa ya bure”.

Akabainisha kuwa: “Ratiba ya matangazo ilikuwa na vipengele vingi, kikosi kimefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanarusha matukio mubashara ya ziara hii, na kufikisha ujumbe wake dunia nzima, swala hili lipo katika mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu sekta ya habari”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: