Kumaliza moja ya hatua muhimu za ukarabati wa mlango wa Imamu Kadhim (a.s) kwa ndani

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kukamilika moja ya hatua muhimu za ukarabati wa mlango wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s) kwa ndani, ni moja ya milango maalum ya wakina mama, unaungana na mlango wa mgahawa (mudhifu) wa Ataba tukufu, uliopo upande wa kusini magharibi ya uwanja wa haram, umetengenezwa kisasa sawa na milango mingine mikuu.

Rais wa kitengo tajwa hapo juu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema kuwa: “Hakika mlango wa Imamu Kaadhim (a.s) unatofautiana na milango mingine ya Ataba tukufu, hautokea katika uwanja wa haram moja kwa moja, bali unatokea kwa pembezoni, jambo ambalo limepelekea kuandaa muundo unao endana na umbo lake, kwa namna ambayo inaendana na milango mingine mikuu katika Ataba tukufu, milango yote inaelekea katika uwanja wa haram takatifu, na imejengwa kisasa”.

Akaongeza: “Tumemaliza hatua muhimu ya kuweka marumaru katika eneo la mlango huo linalo fungamana na mlango mkuu wa haram takatifu, sambamba na kumaliza kazi zote za ufungaji wa vifaa vya umeme pamoja na ukarabati wa ukuta, na kuweka marumaru za ukutani zinazo unganika na sehemu itakayo wekwa Kashi-Karbalai katika hatua ya mwisho ya ujenzi huo”.

Akabainisha kuwa: “Tumeweka marumaru ya kawaida, ujenzi huu umezingatia mambo mengi, ikiwa ni pamoja na muinuko wake kutoka usawa wa uwanja wa haram, na kupafanya kuwa sawa kwa matembezi, kazi iliyo baki ni kuweka Kashi-Karbalai kwenye kuta zake tu, sehemu za kuweka Kashi-Karbala tayali zimesha andaliwa pamoja na sehemu zitakazo wekwa mapambo”.

Kumbuka kuwa kazi hii ni sehemu ya mradi wa ukarabati wa milango ya haram tukufu (ambayo zamani ilikua ndio milango mikuu), pamoja na kuowanisha sehemu ya nje na ndani katika milango hiyo, kwa kuzingatia ramani maalum ya kila mlango inayo endana na jengo takatifu la Ataba pamoja na milango mingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: