Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake: imetangaza kuhitimu kikosi kipya cha wanafunzi wa semina ya Imamu Ridhwa (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuhitimu wanafunzi (22) wa semina ya Imamu Ridhwa (s.a), semina maalum ya kufundisha hukumu za usomaji wa Quráni.

Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi amesema kuwa: “Semina hii inalenga kufundisha utamaduni wa kufuata mafundisho ya Quráni kwa wanawake, wanafunzi wote walio shiriki kwenye semina hii wameanza kuhifadhi Quráni tukufu, baada ya kufaulu mitihani ya mwisho iliyo andaliwa katika semina hiyo”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inajukumu la kufundisha elimu ya Dini kwa wanawake, na miongoni mwa elimu hizo ni (maarifa ya Quráni), sambamba na kuandaa kizazi cha wasomi wanaoweza kufanya tafiti katika sekta tofauti za Quráni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: