Ugeni kutoka wizarani umetembelea chuo kikuu cha Al-Ameed kuangalia majengo yake na mfumo wa ufundishaji

Maoni katika picha
Ugeni kutoka wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu umetembelea chuo kikuu cha Al-Ameed, na kukutana na rais wa chuo hicho pamoja na wakufunzi, kwa lengo la kukagua majengo, maabara na kumbi za madarasa.

Ugeni huo umetembelea maabara na kumbi za madarasa, pamoja na kukagua vifaa vya ufundishaji vinavyo milikiwa na chuo kutoka sehemu tofauti duniani, sambamba na kuangalia mfumo wa elimu masafa na kuongea na wasimamizi wa mfumo huo.

Aidha wameangalia mhadhara wa kielimu unaotolewa kwa wanafunzi kupitia njia ya mtandao chini ya kitengo cha mtandao.

Mwisho wa ziara yao wamepongeza ubora wa majengo ya chuo pamoja na vifaa bora na vya kisasa vinavyo milikiwa na chuo, vinasaidia kupata wanafunzi wenye uwezo mzuri wa kujenga taifa.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya kazi kubwa ya kuboresha uwezo wake katika sekta ya elimu, utamaduni, malezi na tafiti za kielimu hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: