Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeunda kikosi cha kupuliza dawa na kimechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi

Maoni katika picha
Toka mwaka mpya wa masomo ulipo anza chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeunda kikosi cha kupuliza dawa katika maeneo yote ya chuo hadi maofisini, ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi kwa ajili ya kulinda usalama wa wanafunzi, wakufunzi na watumishi kutokana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Kiongozi mtendaji wa chuo Dokta Alaa Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Jambo hili ni muendelezo wa hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona zinazo chukuliwa na chuo hicho katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, sambamba na utekelezaji wa maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu na kamati ya kupambana na maambukizi”.

Akasema: “Kazi ya kupuliza dawa hufanywa kila wakati chini ya ratiba maalum, na kwa kutumia vifaa vilivyo idhinishwa na idara ya afya, bila kuathiri ratiba ya wanafunzi, kazi hiyo inasimamiwa na idara ya madaktari”.

Akamaliza kwa kusema: “Hali kadhalika tumezingatia umbali kati ya mtu na mtu katika ukaaji na kutumia vitakasa mikono pamoja na kuvaa barakoa, na mambo mengine yanayo saidia kuzuwia maambukizi, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu mfululizo kuhusu njia za kujikinga na maambukizi”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kupitia mkakati wake wa kujikinga na maambukizi kimesha chapisha vipeperushi vingi vinavyo elezea virusi vya Korona na namna ya kujikinga navyo, sambamba na kutekeleza maelekezo yote ya kiafya yaliyo tolewa na mamlaka zinazo husika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: