Kuendelea kufanikiwa kwa upasuaji wa kukata na kupunguza utumbo mnene katika hospitali ya rufaa Alkafeel

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limetangaza kuwa limeendelea kufanya kwa mafanikio upasuaji wa kukata utumbo (sleeve gastrectomy) kwa watu wenye tatizo la uzito wa kupindukia, vifaa bora vya kisasa vilivyopo katika hospitali ndio sababu kubwa ya kufanikisha upasuaji huo.

Daktari bingwa wa upasuaji Dokta Swabahi Husseini amesema kuwa: “Tunaendelea kufanya upasuaji wa kukata utumbo (sleeve gastrectomy) katika hospitali ya rufaa Alkafeel, tumepata mafanikio makubwa kwa watu wanye tatizo la unene kupindukia kutoka mikoa tofauti ya Iraq. Akasema kuwa upasuaji huo unahitaji uwezo mzuri wa madaktari na vifaa-tiba bora vya kisasa, navyo vinapatikana katika hospitali ya rufaa Alkafeel, vifaa hivyo ndio vinavyo tuhamasisha sisi kufanya upasuaji huo kama madaktari bingwa”.

Akaongeza kuwa: upasuaji wa kupunguza utumbo kwa kutumia Naadhuur unafanywa na hospitali kubwa nyingi, upasuaji huo unaepusha hatari nyingi kwa mgonjwa, kwani hauhitaji kupasua sehemu kubwa ya muili wa mgonjwa.

Akasema: watu wanene ambao hufanyiwa upasuaji huo, hukutanishwa na madaktari bingwa na kufanyiwa uchunguzi ili kubaini haja ya kufanyiwa upasuaji, na inapo onekana kuwa kuna haja hiyo hufanyia na kubaki chini ya uangalizi wa madaktari kwa muda.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa, chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa fani mbalimbali kila baaada ya muda, pamoja na kupokea wagonjwa walio katika hatua tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: