Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu inawapa mitihani wanafunzi wa Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu inatoa mtihani kwa wanafunzi wa sauti na naghma kupitia kamati ya elimu katika, wanafunzi wamesikilizwa sauti zao na naghma pamoja na kuwafanyia mchujo.

Walifundishwa sauti na naghma wakati wa visomo tofauti vya Quráni tukufu, na kufafanua namna za usomaji na aina za naghma.

Mtihani huu ni sehemu ya ufuatiliaji wa masomo yanayo tolewa na Maahadi ya Quráni tawi la Najafu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imezowea kutoa mafunzo mbalimbali ya Quráni tukufu kila mwaka, lakini kutokana na mazingira ya mwaka huu tumetosheka na program hii ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: