Atabatu Abbasiyya tukufu imeimarisha utekelezaji wa kanuni za kujikinga na maambukizi

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeimarisha utekelezaji wa kanuni za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, baada ya kuongezeka kiwango cha maambukizi katika siku za hivi karibuni, idara ya madaktari imechukua hatua kadhaa za kujikinga na maambukizi, na kulinda usalama wa mazuwaru na watumishi, ikiwa ni pamoja na kupuliza dawa, kazi inayo fanywa na kikosi maalum cha kujikinga na maambukizi kilicho undwa tangu siku za kwanza kabisa lilipo gundulika janga hili.

Haya yamesemwa na kiongozi wa idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Osama Abdul-Hassan, akaongeza kuwa: “Mkakati wa kupambana na virusi vya Korona hauja simama tangu janga hili lilipoanza, tunafanya kazi chini ya maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya kupitia kamati inayo husisha vitengo na idara tofauti za Ataba, baada ya kuongezeka idadi ya maambukizi hivi karibuni, tumeimarisha utekelezaji wa kanuni za kujikinga na maambukizi kwa kufuata muongozo na maelekezo ya kamati ya kupambana na maambukizi ya serikali”.

Akafafanua kuwa: “Tahadhari zote za kujikinga na maambukizi zinatekelezwa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na tumeandaa jengo maalum la Alhayaat kwa ajili ya kutibu watu watakao ambukizwa miongoni mwa watumishi wa Ataba, sambamba na kikosi cha wataalam chenye jukumu la kutoa huduma ya awali kwa mtu yeyote atakaehisiwa kuwa na maambukizi sawa awe zaairu au mtumishi, watamchukua mara moja kwa kutumia gari maalum zilizo andaliwa kwa shughuli hiyo na kumpeleka katika kituo cha afya cha Ummul-Banina (a.s), kisha anapelekwa katika kituo maalum cha kushughulikia watu wenye tatizo hilo”.

Akabainisha kuwa: “Tulianza kazi hii muda mrefu na bado tunaendelea, tumeandaa sehemu ya kuhudumiwa watumishi na mazuwaru kupitia vituo vya ukaguzi kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karbala, sambamba na kuchukua tahadhari za kujikinga na maammbukizi, kama vile kupuliza dawa, kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kutoa maelekezo ya kujikinga na maambukizi”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, pamoja na kufanyia kazi maelekezo yote yaliyo tolewa na idara ya afya, katika ngazi ya Ataba takatifu, mkoa na taifa kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: