Atabatu Abbasiyya yakaribisha mazazi ya kiongozi wa waumini (a.s) kwa kuweka mauwa na maneno ya shangwe na furaha

Maoni katika picha
Alizaliwa katika haram ya Mola na amani yake, na nyumba hifadhio lake na msikiti.

Akiwa mweupe msafi wa nguo mkarimu, kapendeza mzazi wake na mzaliwa.

Atabatu Abbasiyya tukufu inapokea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa pambo la Dini na kiongozi wa waumini na bwana wa wachamungu Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), ambaye mazazi yake yanasadifu siku ya kesho Alkhamisi mwezi kumi na tatu Rajabu.

Kuta za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na korido zake takatifu zimepambwa vizuri na kuwekwa mabango yenye jumbe nzuri za kupongeza mazazi hayo na kutaja sifa na utukufu wa kiongozi wa waumini (a.s), hali kadhalika zimewashwa taa za rangi katika eneo lote linalo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kuweka mauwa na miti ya mapambo katika milango ya haram tukufu.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya takatifu kila mwaka huandaa ratiba maalum ya kuadhimisha tukio hili, huwa na vipengele mbalimbali, lakini kutokana na mazingira ya mwaka huu na kuheshimu maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na kamati ya kujikinga na maambukizi, ya kuepuka mikusanyiko ya watu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Korona, maadhimisho haya yatakua na vitu vichache vitakavyo vanywa kwa kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu au kwa njia ya mtandao, kama inavyo elekezwa na mamlaka zinazo husika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: