Maahadi ya Quráni tukufu inafanya nadwa kuhusu njia za ufundishaji wa Quráni na makosa ambayo hutokea katika usomaji

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya kupitia tawi lake katika wilaya ya Hindiyya mkoani Karbala, imefanya nadwa chini ya anuani isemayo: (Njia za ufundishaji wa Quráni na makosa ambayo hutokea katika usomaji), mkufunzi alikua ni Shekh Muhammad Fahami Usfuur kutoka nchini Misri, imehudhuriwa na kundi la walimu na wadau wa Quráni.

Nadwa imefanywa chini ya utekelezaji wa tahadhari za kujikinga na maambukizi ndani ya ofisi ya tawi la Maahadi, imefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na Yusufu Fatalawi, ukafuata ujume wa makaribisho uliotolewa na Uastadh Mustwafa Mussawi ambaye ni mmoja wa walimu wa tawi.

Kisha Mhadhiri akaeleza ratiba ya nadwa, akaeleza mambo mengi muhimu kuhusu njia za ufundishaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu, na hatua za kielimu anazotakiwa mwalimu kuzifuata, ili kufikia katika lengo na kupata matokeo mazuri, aidha akaeleza baadhi ya makosa ambayo hufanywa mara nyingi katika usomaji wa Quráni na namna ya kujiebusha na makosa hayo, pia akaeleza namna ya kusoma maqaamu na kuchunga matamshi ya herufi pamoja na mambo mengine yanayo saidia usomaji mzuri wa Quráni na kumuwezesha msomaji kutafakari maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu, akafafanua pia aina za usomaji wa Quráni na akabainisha visomo mashuhuri.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Hindiyya inaendelea na ratiba ya kufanya nadwa mbili kila mwezi, chini ya uhadhiri wa wasomi wa hauza na sekula, na huhudhuriwa na wadau wengi wa Quráni tukufu, na kutoa elimu kubwa ya kuvitambua vizito viwili Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: