Shirika la Alkafeel limeanza kulima aina mpya ya ngano

Maoni katika picha
Shirika la Alkafeel limeanza kuandaa shamba la kupanda aina mpya za ngano, huu ni muendelezo wa mafanikio yaliyo fikiwa siku za nyuma katika sekta ya kilimo.

Mkuu wa shirika la Alkafeel Mhandisi Rasuul Rumahi amesema kuwa: “Baada ya mafanikio yaliyo patikana katika mashamba, juhudi zimeelekezwa katika kulima aina mpya ya ngano (aina ya Uturuki Romeli) nayo imeandikwa kwa jina la shirika.

Akaongeza kuwa: “Mashamba ya kumwagilia hupewa umuhimu mkubwa na shirika la Alkafeel la Atabatu Abbasiyya pia ni moja ya mradi wenye kutoa mavuno makubwa ya mazao ya kimkakati, likiwemo zao la ngano lenye mchango mkubwa katika kulisha soko ya ndani”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inalenga kuboresha sekta ya kilimo hapa nchini, kwa kutumia njia za kisasa zinazo weza kuleta mapinguzi makubwa katika kilimo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: