Kumbukumbu ya mwaka wa tano: Katika siku ya kuzaliwa baba yake ulifanyika uzinduzi wa dirisha la malalo yake takatifu chini ya utendaji wa watumishi

Maoni katika picha
Leo ni siku ya kumbukumbu ya mwaka wa tano toka kuzinduliwa kwa miradi muhimu uliofanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa mafundi wa kiwanda cha kutengeneza madirisha ya makaburi matukufu na milango yake, nalo ni dirisha la malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), lililo zinduliwa usiku wa mwezi kumi na tatu Rajabu mwaka wa 1437h.

tukio hilo tukufu lilifanywa katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), ulipo fanywa uzinduzi wa dirisha jipya la kihistoria la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi iliyofanywa na watumishi wake na inafaa kuandikwa kwa herufi za nuru.

Tukio hili la kihistoria lilisubiriwa na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), walikua na kiu ya kuangalia na kugusa dirisha hilo la kaburi takatifu, tukio litakalo andikwa katika historia kwa herufi za dhahabu, ukizingatia kuwa dirisha hilo limetengenezwa na mikono ya watumishi wake wanao fanya kazi katika kiwanda cha madirisha ya makaburi na milango mitakatifu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanya kila wawezalo kuhakikisha linakuwa bora zaidi, na lenye kuendana na hadhi ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mafanikio hayo ya kiufundi ni sehemu ya mafanikio ya Atabatu Abbasiyya na wasimamizi wake.

Huu ni mradi wa kihistoria wenye umuhimu mkubwa kwani ndio dirisha la kwanza kutengenezwa hapa Iraq, tena lenye ubora mkubwa kuzidi madirisha yote ya makaburi matakatifu, yaliyo tengenezwa kwenye miaka ya sitini karne iliyopita.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kwenye ujembe wake wakati wa uzinguzi wa dirisha hilo alisema kuwa: “Hakika watumishi wa kiwanda cha kutengeneza madirisha wamefanya kazi kubwa itakayo pongezwa katika historia, wamethibitisha uwezo wa raia wa taifa hili, hakika malipo yao yapo kwa Mwenyezi Mungu”.

Naye rais wa wakfu Shia Sayyid Alaa Mussawi, alisema kuwa: “Kufanikisha utengenezaji wa dirisha hili umetimiza ndoto na matarajio ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) pamoja na wapenzi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ni fahari kubwa kwa kila mtu na wairaqi wote kwa ujumla, aidha ni fahari kwa Ataba na fahari kwa waumini wote”.

Dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s) ndio dirisha zuri zaidi, limetengenezwa kwa umaridadi mkubwa na kuwekwa nakshi nzuri tofauti na zilizo kuwepo pamoja na kufanyiwa baadhi ya mabadiliko kwa kutumia ufundi wa kiiraq sehemu nyingi za nje, ama upande wa ndani ya dirisha ubunifu na ufundi wote uliotumika ni wenye asili ya Iraq, zimetumika zaidi ya aina saba za mbao za asili zilizo nakshiwa kwa aya za Quráni tukufu, na kutengenezwa na watumishi watukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kuna mambo mengi yamelifanya dirisha hili kuwa la pekee, ikiwa ni pamoja na kutumia mbao za Burma katika kutengeneza umbo la mbao, nazo ni aina bora zaidi, na kutengeneza baadhi ya sehemu kwa dhahabu yenye ujazo wa gram (22) ambazo zilikua zimetengenezwa kwa fedha na kuchovya dhahabu, fedha halisi iliyo tumika ni karibu (kilo 2,750) huku dhahadu ikitumika jumla ya (kilo 411), sehemu nyingi zimeongezwa ujazo wa dhahabu kwa zaidi ya asilimia kumi, ili kulifanya kuwa imara, na kulipa hadhi na heshima kubwa, umetumika umaridadi mkubwa na ufundi wa hali ya juu katika kutengeneza sehemu nyingi za dirisha hili tukufu nje na ndani, sambamba na kulinda uzuri wa dirisha hilo takatifu, kazi hiyo tukufu ilifungua milango ya kutengeneza madirisha ya makaburi na mazaru zingine za ndani na nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: