Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu umegawa zaidi ya sahani (1500) za chakula kwa familia zinazo athiriwa na marufuku ya kutembea

Maoni katika picha
Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) umegawa zaidi ya sahani za chakula (1500) kwa familia zilizo athirika na marufuku ya kutembea hapa mkoani, na wamegawa kwa jina wa bibi Zainabu (a.s) ambaye siku ya kifo chake inasadifu leo.

Rais wa kitengo cha mgahawa Mhandisi Aadil Hamami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kama kawaida ya mgahawa hugawa chakula katika siku za matukio ya kidini, sawa liwe tukio la kuzaliwa au kifo cha Imamu mtakatifu (a.s), huwapa chakula mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na marufuku ya kutembea inayo sababisha kukosekana mazuwaru, na kufuatia maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, mgawaha umegawa chakula kwa familia zilizo athiriwa na marufuku ya kutembea”.

Akaongeza kuwa: “Tumeandaa chakula tangu asubihi na kuviweka kwenye vifungashi maalum kisha tumesambaza kwa mafakiri wa Karbala kwa kutumia magari”.

Kumbuka kuwa mgahawa umegawa chakula pia kwa askari wa mkoa wa Karbala wanao simamia marufuku ya kutembea pamoja na kwenye vituo vya kupambana na maambukizi ya virusi kwa Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: