Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea na kazi ya kukarabati kituo cha afya katika kitongoji cha Shalamijah

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea na kazi ya ukarabati wa kituo cha afya katika kitongoji cha Shalamijah kilichopo mashariki ya mkoa wa Basra karibu na mpaka wa Iran.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Samiri Abbasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi hiyo inafanywa hivi sasa, ilianza baada ya kupokea maombi ya kukarabati kituo hicho kutoka idara ya afya ya mkoa wa Basra, ndipo tukaunda kamati ya kufanya upembuzi yakinifu na kuandika mahitaji kwa ajili ya kuanza matengenezo haya”.

Akaongeza kuwa: Ukarabati umehusisha sehemu nyingi za kituo cha afya, kama ifuatavyo:

  • - Kukarabati kumbi tisa na kuweka vifaa vyote vinavyo hitajika kwa mujibu wa vigezo vya afya pamoja na vifaa-tiba.
  • - Kutengeneza njia kuu na ndogo pamoja na kuweka zege au lami.
  • - Kukarabati nyumba za chini na mifumo ya (umeme, maji, zimamoto, kamera na vyoo).
  • - Kutengeneza sehemu ya kupumzika na kupokea wageni yenye ukubwa wa mita (550).

Akamaliza kwa kusema: “Kazi zote zinaenda kama zilivyo pangwa, tunafanya kazi saa (12) kila siku”.

Kumbuka kuwa kazi ya kukarabati kituo hiki ni sehemu ya ratiba ya miradi ya kibinaadamu inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, pia ni sehemu ya mkakati wa kukarabati majengo ya serikali yaliyopo katika hali mbaya, miongoni mwa majengo hayo ni shule, taasisi za kibinaadamu na vituo vya afya ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: