Kukamilika ukarabati wa kituo cha afya katika kitongoji cha Shalamijah kilichopo mpakani

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesema kuwa mafundi wake wamemaliza ukarabati wa kituo cha afya katika kitongoji cha Shalamijah kilichopo mpakani mwa Iraq na Iran mashariki ya mkoa wa Basra, mafanikio hayo yanaingizwa katika orodha ya ujenzi wa vituo vilivyo jengwa katika mazingira ya maambukizi ya virusi vya Korona, na kusaidia sekta ya afya.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Samiri Abbasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi hii imefanywa baada ya kupokea maombi kutoka idara ya afya ya mkoa wa Basra ya kutaka kukarabatiwa kituo hicho, kwani ni kituo muhini na moja ya vituo vinavyo pima watu wanao ingia nchini, baada ya kupata idhini kutoka kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, tuliandaa kamati ya wataalamu waliofanya upembuzi yakinifu na kuandika mahitaji ya ukarabati huo kisha tukaanza kazi”.

Akaongeza kuwa: “Sehemu nyingi za kituo zimefanyiwa ukarabati, tumekarabati kumbi tisa, kwa kutengeneza dari na kuweka marumaru za kutani na za chini, pamoja na kuweka vitu vyote muhimu vinavyo hitajika katika kumbi hizo, na kuzifanya kuwa na muonekano mpya unao endana na mazingira ya jengo”.

Akabainisha kuwa: “Ukarabati huo umehusisha pia utengenezaji wa njia kuu na ndogo kwa kuweka zege au lami, sambamba na kukarabati mfumo wa (umeme, maji, zima moto, kamera na vyoo) na kutengeneza uwanja wa kupumzika na kupokea wageni wenye ukubwa wa mita (550)”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunamshuru Mwenyezi Mungu kazi imekamilika ndani ya muda uliopangwa, tumetumia siku (13) kwa kufanya kazi saa (12) kila siku”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: