Marjaa Dini mkuu: Yawapasa viongozi wakuu wa Dini kutatua changamoto za wananchi hususan raia wa Palestina

Maoni katika picha
Mheshimiwa Ayatullahi mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, alipokutana na Papa mkuu (Papa wa Vatkani) amezungumzia changamoto walizo nazo raia wa mataifa tofauti, na akahimiza umuhimu wa viongozi wa Dini na kiroho kusaidia kutatua changamoto za raia hao.

Lifuatalo ni tamko lililotolewa na ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu Asubuhi ya Jumamosi mwezi (21 Rajabu 1442h) sawa na tarehe (6 Machi 2021h): Mheshimiwa Sayyid ameongea kuhusu changamoto iliyopo katika mataifa mbalimbali, dhulma, ukatili, ufakiri, ubaguzi wa kidini, kifikra na kutoweka uadilifu katika jamii, hususan chamgamoto inayo zikumba nchi zetu, vita, ugaidi, vikwazo vya kiuchumi na mengineyo, bila kusahau mateso makubwa wanayopata raia wa Palestina katika ardhi inayokaliwa kimabavu.

Akaashiria nafasi kubwa ya viongozi wa Dini na kiroho katika kutatua changamoto hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: