Marjaa Dini mkuu asisitiza kuwa wakristo wanapewa haki zote za kikatiba

Maoni katika picha
Mheshimiwa Ayatullahi mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani alipo kutana na Papa mkuu (Papa wa Vatkani), ameonyesha matumaini ya kuhakikisha wakristo wanatendewa haki kwa mujibu wa katika na kuishi sawa na raia wengine wa Iraq, na kazi kubwa iliyofanywa na Marjaa Dini mkuu katika kuwahami wakati wa vita za miaka ya nyuma.

Lifuatalo ni tamko lililotolewa na ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu asubuhi ya Jumamosi mwezi (21 Rarabu 1442h) sawa na tarehe (6 Machi 2021m):

Akaongea kuhusu nafasi ya Iraq na historia yake tukufu pamoja na ukarimu wa raia wake wenye mitazamo tofauti, akawaombea kushinda mtihani walionao ndani ya muda mfupi, na akaonyesha matumaini ya wakristo wa taifa hili ya kuishi sawa na raia wengine wa Iraq chini ya misingi ya katiba, akasifu nafasi ya Marjaa Dini mkuu na namna alivyo simama imara kuwahami pamoja na wananchi wengine wote wakati wa vita iliyopita, hususan baada ya miji mingi ya Iraq kuvamiwa na magaidi, waliokuwa wanafanya jinai kubwa zisizo elezeka. Mheshimiwa Papa mkuu na wafuasi wa kanisa Katoliki wakaomba kheri na utulivu kwa binaadamu wote, na akapewa pole ya uchovu wa safari ya kuja Najafu katika ziara hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: