Warsha ya kiofisi imeratibiwa na kitengo cha maendeleo endelevu

Maoni katika picha
Kitengo cha maeneleo endelevu kimeratibu warsha ya mambo ya kiutawala, walengwa wa warsha hiyo ni watumishi wa shirika la Nurul-Kafeel, inalenga kuwajengea uwezo wa utendaji wa majukumu yao ndani ya taasisi inayokua.

Tumeongea na rais wa kitengo cha maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Muhammad Hassan Jaabir kuhusu warsha hiyo, amesema kuwa: “Kitengo cha maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya warsha ya (mambo ya mawasiliano na khutuba rasmi) kwa watumishi wa shirika la Nurul-Kafeel, kwa muda wa siku nne, kila siku washiriki wamefundishwa kwa muda wa saa tatu, kulikua na washiriki (25)”.

Akaongeza kuwa: “Warsha inalenga kujenga uwezo kwa washiriki wa kuandaa ujumbe na ripoti za kiofisi, pamoja na kuwafundisha mambo ya kiutawala sambamba na kujiepusha na makosa ya kilugha, pamoja na kuandaa ujumbe na khutuba rasmi zinazo endana na haiba pamoja na heshima ya idara husika”.

Akafafanua kuwa: “Warsha ilikua na mada nyingi, zikiwemo: (Uwelewa wa khutuba rasmi, fani za uandishi, kanuni saba za uandishi wa ujumbe rasmi, zana zilizopo katika mitandao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: