Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkaadhim (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya Husseiniyya imeratibu majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Mussa bun Jafari (a.s), itakayo fanyika Jumatano mwezi (25 Rajabu 1442h), majlisi hiyo itafanyika kwa siku tatu na kila siku itakua na mihadhara miwili, asubuhi na jioni, ndani ya ukumbi wa Aljuud kwa kufuata kanuni zote za kujikinga na maambukizi.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara Shekh Abduswahibu Twaiy, amesema: “Majlisi hizo ni miongoni mwa mradi wa Ummul-Banina (a.s) unaohusika kwa kiasi kikubwa na shughuli za kuhuisha tarehe za vifo na kuzaliwa kwa Maimamu (a.s), ikiwemo kumbukumbu ya kifo cha mtu mwenye sijida ndefu Imamu Mussa bun Jafari (a.s), kama kawaida katika kuadhimisha tukio hili majlisi zimewekwa katika nyakati mbili, wakati wa subuhi itaongozwa na Shekh Kaadhim Asadi, na wakati wa jioni itaongozwa na Shekh Rafidi Tamimi”.

Akaongeza: “Mihadhara itatolewa na wahadhiri wawili wataongea kuhusu historia ya Imamu huyu mtakatifu (a.s), histori inayo onyesha namna alivyo fuata mwenendo wa baba yake Imamu Jafari Swadiq (a.s), alivyo simama imara kuzuwia mitazamo potofu iliyokuwa inasambazwa katika ulimwengu wa kiislamu wakati ule, pamoja na kuongelea maisha ya Imamu yaliyojaa ibada na msimamo imara katika kusimamia haki, pamoja na subira kubwa ya maudhi aliyokua akifanyiwa na watawala wa zama zake, walimfanyia manyanyaso ya kila aina, hadi wakamteka na kumfunga katika jela mbaya zaidi baada ya kumtoa katika mji wa babu yake na kumleta Iraq".
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: