Kifo cha bwana wa Batwihaa Muumini wa kikuraishi Abu Twalib (a.s)

Maoni katika picha
Imepokelewa kuwa jemedari wa kiislamu alikufa –mwezi ishirini na sita Rajabu mwaka wa kumi wa utume-, Ammi wa Mtume (s.a.w.w) Abu Twalib (r.a), Muumini wa kikuraishi na mlinzi wa Mtume, mlezi wake baada ya baba yake.

Jina lake ni Abdulmanafi bun Abdulmutwalib bun Hashim, na kuniya yake ni Abu Twalib, alizaliwa kabla ya kuzaliwa Mtume (s.a.w.w) kwa miaka thelathini na tano, alikuwa bwana wa Batwihaa na Shekh wa makuraishi na rais wa Maka, alimuowa Fatuma binti Asadi, alikuwa Hashimiyyu wa kwanza kumuowa mwanamke wa Hashimiyyah, akamzaa katika wanaume: Twalibu (ambaye huitwa kwa jina lake) na Aqiil, Jafari, Ali, na katika wanawake: Ummu Haani jina lake ni (Fakhitah) na Jumanah.

Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipoanza kulingania umma Dini tukufu, Abu Twalib alimuamini na akasadikisha mafundisho yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu, lakini hakudhihirisha Imani yake, aliificha ili aweze kumnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) pamoja na watakao kuwa pamoja nae.

Shekh Mufidi anasema: Imamiyya wamekubaliana kuwa wazazi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuanzia Adam hadi Abdullahi bun Abdulmutwalib walikuwa wanamuamini Mwenyezi Mungu mtukufu, walikuwa ni watu wa tauhidi. Pia Ammi yake Abu Twalib (r.a) alikufa akiwa ni Muumini, na mama yake Amina bint Wahabi alikuwa ni mtu wa tauhidi atafufuliwa pamoja na waumini”.

Shekh Swaduqu anasema: “Tunaamini kuwa wazazi wa Mtume walikuwa waislamu kuanzia Adam hadi baba yake Abdullahi, hakika Abu Twalibu alikuwa muislamu, na mama yake Amina bint Wahabi alikuwa muislamu”.

Abuu Baswiri Liith Almuraadi anasema: “Nilimuambia Abu Jafari (a.s) bwana wangu, watu wanasema kuwa: Abu Twalib yupo katika moto mkali sana unachemsha ubongo wake! Akasema (a.s): Wallahi wamesema uongo, hakika Imani ya Abu Twalib lau ikiwekwa upande mmoja na mzani na Imani ya waja wengine wote katika upande wa pili wa mzani, Imani ya Abu Twalib izakuwa nzito kushinda Imani zao, kisha akasema: Alikuwa ni kiongozi wa waumini, alikuwa anaamrisha kufanyiwa hija baba wa Mtume na mama yake (s.a.w.w), Abu Twalib alikuwa mlinzi wa Mtume, aliusia wafanyiwe hija baada ya kufa kwake”.

Imamu Swadiq (a.s) anasema: “Jibrilu (a.s) alikuja kwa Mtume (s.a.w.w) akasema: ewe Muhammad, hakika Mola wako anakutumia salam na anasema: Mimi nimeharamisha moto kwa mgongo ulio kuhifadhi na tumbo lililo kubeba, na miguu iliyo kulea, mgongo ulio kuhifadhi ni baba yako Abdullahi bun Abdulmutwalib, na tumbo lililo kubeba ni mama yako Amina bint Wahabi, na miguu iliyokulea ni Abu Twalib”.

Alipokufa (r.a) kiongozi wa waumini (a.s) alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w), akampa taarifa ya kifo, Mtume (s.a.w.w) akaumia sana kwa taarifa hiyo, akasema: Ewe Ali nenda kasimamie kumuosha na kumvisha sanda (maziko), kiondozi wa waumini akafanya kama alivyo agizwa, alipo muinua kitandani, Mtume (s.a.w.w) akamkumbatia na akasema: (Uliunga undugu, na umelipwa kheri, ulinilea na kunitunza nilipokua mdogo, na ulinilinda na kuninusuru nilipokua mkubwa).

Kisha akawageukia watu na akasema: (Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, nitamuombea samahani Ammi yangu isiyowezwa na vizito viwili).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: