Maahadi ya Quráni tukufu imesema: Ratiba ya Kadhimiyya imekuwa na mafanikio

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tawi la Bagdad chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefungua vituo kadhaa vya kufundisha usomaji wa Quráni kwa mazuwaru waliokuwa wakielekea katika eneo takatifu la Kadhimiyya, kuomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s) mwezi 25 Rajabu.

Tumeongea na mkuu wa tawi hilo Ustadh Nabiil Saaidi amesema kuwa: “Huwa tunafungua vituo vya usomaji sahihi wa Quráni tukufu kwa mazuwaru, katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ambapo huwasomesha sura fupi na maneno ya kuswalia”.

Akaongeza kuwa: “Mradi huu umefanyika siku zote za ziara kwa kuzingatia kanuni zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, mwaka huu zaidi ya mazuwaru elfu nne wamenufaika na ratiba hii”.

Tambua kuwa asilimia kubwa ya wanufaika wa ratiba hii ni vijana wenye umri mdogo na watu wasiojua kusoma.

Kumbuka Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Bagdad inaendelea na harakati za kufundisha Quráni kwa kuzingatia kanuni za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, nayo ni moja ya matawi ya Maahadi ya Quráni chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, aidha ni moja ya vituo muhimu vya kusambaza utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Quráni tukufu kwa watu wa rika tofauti ndani ya jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: