Kuanza kusajili wa kushiriki katika semina ya uimbaji

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kusajili washiriki wa semina ya uimbaji wa kaswida zinazo husu Imamu Husseini (a.s), inayo tarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Shabani, semina hiyo itaendeshwa kwa njia ya mtandao, inalenga kukuza kipaji cha uimbaji kwa wasichana wenye umri wa miaka (13 – 18), sambamba na kuibua vipaji vyao na kuwapa muongozo sahihi, nayo ni miongoni mwa semina zinazo fanywa na Jumuiya katika kipindi hiki.

Mada kubwa zitakazo fundishwa ni:

  • - Historia ya uimbaji.
  • - Adabu za uimbaji.
  • - Mahadhi (maqaamaat).

Watu watakao shishiki kwenye semina hii watapewa vyeti vya ushiriki baada ya kufanya mtihani wa mwisho, pamoja na kutoa zawadi kwa washiriki bora, mshiriki ataweza kupata mhadhara wakati wowote na akiwa mahala popote, kuna App itakayo tengenezwa wakati wa semina, watakao fanya vizuri katika semina hii watapewa nafasi ya kushiriki katika semina zijazo.

Yeyote anayependa kushiriki ajaze fomu ya kujisajili kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/LoicKig4vVb84jWm8
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: