Makumbusho ya Alkafeel hutunza vipi miswala?

Maoni katika picha
Makumbusho ya vifaa na nakala-kale Alkafeel inazaidi ya miswala (1000) ya aina mbalimbali na ukubwa tofauti, baadhi yake ni ya kifahari zaidi na historia yake inarejea miongo tofauti, imewekwa nakshi, mapambo, picha na mengineyo, walio tengeneza miswala hiyo walifanya kazi kubwa na walitumia weledi wa hali ya juu, watumishi wa makumbusho nao wanafanya kila wawezalo katika kuitunza na kuzingatia umuhimu wake kihistoria.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa makumbusho ya Alkafeel Ustadh Swadiq Laazim Zaidi, akaongeza kuwa: “Miswala na kazi zingine za mikono zilizopo katika makumbusho ya Alkafeel, ni adimu na haipo katika makumbusho zingine, hii ndio sifa ya pekee katika makumbusho ya Alkafeel, miswala hiyo hutolewa zawadi kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), kuna kamati ya wataalamu inayo simamia kila kipengele cha utunzaji wa miswala hiyo”.

Akasema kuwa: “Miongoni mwa hatua muhimu ambazo kila mswala unapitia baada ya kuupokea kutoka kitengo cha zawadi na nadhiri, mlango pekee wa kupokea zawadi hizo ni:

  • - Kuupiga picha na kuuingiza katika orodha ya vifaa vya makumbusho.
  • - Kufanya vipimo na kufanya matengenezo yanayo hitajika kwa ajili ya utunzaji wake chini ya jopo la wahifadhi waliopobea.
  • - Kuweka namba maalum ya uhifadhi inaitwa (kodi).
  • - Huandaliwa utambulisho maalum wa kila mswala, ambapo huwekwa (picha – aina ya kasoro kama ipo – aina za nakshi na michoro iliyopo – vipimo vya mswala – aina ya mswala – aina ya nyuzi zilizo tumika kusukiwa mswala huo – sehemu ulikotengenezwa na umri wake), taarifa ya kila mswala hutunzwa kwa njia ya elektronik”.

Akamaliza kwa kusema: “Ukarabati na utunzaji wa miswala hufanywa kwa teknolojia za kisasa chini ya jopo la wataalam wa miswala, kila mswala hutunzwa kulingana na aina yake, umri wake na kasoro iliyopo, kisha huwekwa katika stoo ya miswala ambayo mazingira yote huzingatiwa, ikiwa ni pamoja na kiwango cha joto na baridi na mambo mengine ya msingi katika utunzaji wake, pamoja na mambo yote hayo kila baada ya muda hufanyika matengenezo na kuwekwa baadhi ya miswala katika ukumbi wa maonyesho ya makumbusho kwa kufuata ratiba maalum”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: