Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu unatoa pole kwa familia za watu wa Buduur

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka kamati ya maelekezo na msaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea mkoa wa Swalahu-Dini kutoa pole kwa wahanga wa shambulio la kigaidi lililofanywa na magaidi wa Daesh na kupelekea vifo vya watu nane wa familia moja ya kabila la Aali Abbasi kwenye kijiji cha Buduur mkoani Swalahu-Dini.

Kiongozi wa msafara huo Shekh Aaridhwi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumekuja kutoa pole kwa wafiwa walio fanyiwa unyama mkubwa na magaidi wa Daesh, unyama ambao unahuzunisha na kuumiza kila mtu mwenye ubinaadamu, hiyo ndio Dini ya magaidi hao, hawalitakii kheri taifa hili wala hawachagui mtu katika kufanya jinai zao, wanafanya hima ya kuvunja amani na kuondoa utulivu katika taifa hili na raia wake, pamoja na kuwa wananchi wa taifa hili kwa umoja wao walifanikiwa kuwashinda na kukomboa ardhi yote iliyokuwa imetekwa na magaidi hao”.

Akaongeza kuwa: “Ugeni umetoa pole nyingi kwa wafiwa na kusisitiza kuwa huu ni msiba wa kila muiraq, kwani wao ni sawa na muili mmoja, matukio kama haya yasiwavunje moyo wa kuendelea kupambana na adui huyu anayefanya mashambulizi ya uoga, wafiwa wamefurahishwa na tukio hili na wametoa shukrani kwa kila aliyewezesha ziara hii tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: