Watumishi wa malalo ya ndugu yake wanatoa pongezi mbele ya kaburi lake katika kumbukumbu ya mazazi matukufu

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu uliojumuisha wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo pamoja na watumishi, umetoa pongezi kwa Imamu wa zama (a.f) katika kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s), mbele ya kaburi lake leo asubuhi, siku ambayo dunia imenawirika na mauwa yamechanua na malaika wamefurahi kwa mazazi haya matukufu.

Ugeni uliondoka katika malalo ya ndugu yake na mbeba bendera wake Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kumpa pongezi wakiwa wamebeba mauwa, wakatembea kuelekea kwenye kaburi la Imamu Hussein (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wakapokewa na watumishi wa malalo yake takatifu kwa maneno mazuri ya ukaribisho na kupongezana, kisha wakaenda pamoja hadi kwenye kaburi lake takatifu, wakasimama kwa pamoja mbele ya kaburi hilo tukufu wakiwa wameshika mauwa, wakasoma dua ya kulitakia amani na utulivu taifa la Iraq, na awaokoe na balaa la janga hili (Korona) pamoja na nchi zote za kiislamu.

Baada ya hapo ugeni ulikwenda kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai, wakampa salamu za pongezi kutoka kwa watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakiongozwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katika kumbukumbu hii takatifu ya kuzaliwa kwa baba wa watu huru bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: