Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa mwezi wa familia

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya hafla kubwa ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mwezi wa bani Hashim Abulfadhil Abbasi (a.s), ambaye alizaliwa siku kama ya leo mwezi nne Shabani, hafla hiyo imefanywa ndani ya ukumbi mkuu wa Maahadi katika mkoa wa Najafu.

Hafla hiyo ni sehemu ya ratiba iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya katika kuadhimisha tukio hili, imehudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi wa Maahadi pamoja na wageni waalikwa chini ya utekelezaji wa maelekezo ya kujikinga na maambukizi.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi amesema kuwa: “Hakika kongamano hili hufanywa kila mwaka katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), huwa ni sehemu ya kuhuisha ahadi ya utumishi na uaminifu kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Hafla ilikuwa na mambo mbalimbali ya kidini pamoja na kaswida na mashairi yaliyo onyesha shangwe na furaha katika maadhimisho haya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: