Warsha ya kujenga uwezo kuhusu maswala ya usalama wa kemia

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendesha warsha ya usalama wa kemia kwa watumishi wa maabara.

Semina hiyo inahusu njia za kiafya katika kuamiliana na kemia zenye madhara kwa mwanaadamu, tumeongea na Dokta Ahmadi Kaabi rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesema kuwa: “Ili kuboresha huduma na kujikinga na madhara ya kikemia kwa watumishi wa maabara ya Atabatu Abbasiyya, kamati ya sayansi katika kitengo cha malezi na elimu ya juu imeandaa warsha maalum kuhusu usalama wa kemia”.

Akaongeza kuwa: “Tumefanya warsha chini ya anuani isemayo: (Ubainifu wa usalama wa kemia) na (Bakteria zinazo pambana na chembechembe hai) anuani ya tatu ilikuwa inasema (Uongozi bora wa maabara), na nyingine inasema: (Uongozi tofauti wa aina tofauti), warsha imewezeshwa na wakufunzi waliobobea katika sekta hiyo, jambo hili ni muhimu katika ufanisi wa utendaji ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: