Upasuaji wa aina yake.. kurudisha mfupa wa kiuno sehemu yake

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanikiwa kurudisha mfupa wa kiuno sehemu yake (Congenital hip dislocation) kwa mtoto mwenye umri wa miaka sita (6).

Daktari bingwa wa mifupa na viungo katika hospitali ya Alkafeel, Dokta Bariri Muhammad Ali Asadi amesema kuwa: “Madaktari wetu wamefanikiwa kurudisha mfupa wa kiuno sehemu yake kwa mtoto mwenye umri wa miaka sita (6)”.

Akabainisha kuwa: “Mtoto huyo alikuwa na tatizo hilo (Congenital hip dislocation) upande wa kushoto lililo msababishia ulemavu”.

Akaongeza kuwa: “Upasuaji umehusisha kufungua mifupa hiyo na kupunguza sehemu ya mfupa na kusawazisha vizuri mfupa wa paja kwa ndani”.

Akasisitiza kuwa: Anatarajiwa kupona siku chache baada ya upasuaji huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: