Kuanza usajili wa program ya uokozi

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika kitengo cha habari, kwa kushirikiana na idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kufungua mlango wa usajili kwa wanao penda kushiriki katika program ya utoaji wa huduma za uokozi, kwa lengo la kuandaa kikosi cha wanafunzi walio tayali kujitolea katika kutoa huduma za matibabu.

Watakao fundishwa utoaji wa huduma za uokozi, na kupambana na majanga ya aina mbalimbali, ndani na nje ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hususan katika msimu wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Kiongozi wa idara ya watoto na makuzi Ustadh Hassanaini Faruuq amesema kuwa: “Usajili wa kushiriki kwenye mafunzo haya unahusisha wanafunzi wa: (udaktari, udaktari wa meno, famasia na wauguzi), vitivo vingine vitahusika na kazi za kujitolea, baada ya kupata mafunzo watafanya kazi kwa zamu mbili ya asubuhi na jioni, siku ya Akhamisi na Ijumaa kila wiki na katika siku za ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu”.

Akafafanua kuwa: “Program inahusisha watu wenye umri wa miaka (18 – 35), miongoni mwa yatakayo fanywa ni:

  • - Mbini za uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza.
  • - Masomo ya fani mbalimbali.
  • - Hema za Skaut.
  • - Safari za kitalii.
  • - Kuendeleza uwezo na vipaji vya washiriki.
  • - Wanafunzi wa mikoani watapewa malazi.
  • - Wanafunzi watapewa chakula.
  • - Kutakuwa na usafiri wa bure”.

Akafafanua kuwa: “Unaweza kujisajili kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/WF6jc5vSQFT226Gm8

Kwa maelezo zaidi piga simu namba: (07724062987)".
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: