Kukamilika maandalizi ya kongamano la kielimu na kimataifa la tatu

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kukamilika maandalizi yote ya kongamano la kimataifa awamu ya tatu la madaktari na wahandisi, linalo simamiwa na chuo hicho kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-Ameed na hospitali ya Alkafeel pamoja na chuo kikuu cha Malezia (UKM).

Mheshimiwa rais wa chuo cha Alkafeel Dokta Nurisi Muhammad Shahidi Dahani pamoja na wasaidizi wake wawili wamekutana na kamati ya elimu ya kongamano hilo na kujadili ratiba na maandalizi ya kongamano, pamoja na kuangalia toleo la mwisho la tafiti zitakazo shiriki kwenye kongamano.

Hali kadhalika amekagua kumbi zitakazo tumika katika kongamano, pamoja na tahadhari zinazo chukuliwa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya korona ikiwa ni pamoja na ukaaji kwa kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu, na kugawa shughuli kulingana na ukubwa wa kumbi pamoja na mada zitakazo wasilishwa.

Kumbuka kuwa kongamano litafunguliwa siku ya Jumatatu (8 Shabani 1442h) sawa na tarehe (22 Machi 2021m) ndani ya ukumbi wa Shekh Nasru-Dini Tusi katika kitivo cha udaktari wa meno saa nne asubuhi, unaweza kushiriki na kufuatilia kongamano hilo kupitia link ifuatayo:

https://alkafeel-edu-iq.zoom.us/my/iscku
Passcode:
kafeel
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: