Atabatu Abbasiyya tukufu imesaidia zaidi ya watu (2000)

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kukamilika kwa ukarabadi wa moja ya vituo vya kusafisha maji katika kitongoji cha Baniqiya (Nuur) kwenye mkoa wa Najafu.

Kazi hiyo imefanywa baada ya Atabatu Abbasiyya kupokea maombi kutoka kwa wakazi wa kitongoji hicho chenye watu zaidi ya (2000) na nyumba zaidi ya (500), ya kutengenezewa kituo hicho, kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wakazi wa kijiji hicho.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi, Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu imeshafanya miradi mingi inayo lenga kuhudumia wananchi, ikiwemo inayo mlenga mwananchi moja kwa moja, imekuwa ikijitolea kadri ya uwezo wake, miongoni mwa miradi ambayo tumekuwa tukiifanya ni mradi wa maji, tumeanzisha vituo vya usafishaji na usambazaji wa maji (R.O station) sehemu mbalimbali, kikiwemo kituo hiki ambacho maombi ya kutengenezwa kwake yameletwa Atabatu Abbasiyya, ndipo idara ya maji katika kitengo cha miradi ikachukua jukumu la kukitengeneza na kuhakikisha familia hizo zinapata maji safi na salama kwa kunywa”.

Naye msimamizi wa mradi huu Mhandisi Basam Hashimi amesema kuwa: “Baada ya kuagizwa kufanya kazi hii, tuliunda kikosi kazi kilicho fanya upembuzi yakinifu na kubaini vitu vinavyo hitajika, na baada ya kukamilisha vitendea kazi tukaanza matengenezo mara moja kama ilivyo pangwa, hadi sasa kituo kinafanya kazi kwa asilimia (%80), tumebadilisha karibu mitambo (30000) na tayali kinatoa huduma kwa wananchi, tumeondoa vipuli vingi vya zamani na kufunga vipya vyenye uwezo mkubwa sambamba na kuunganisha kituo hicho na chanzo cha maji kinacho endana na ukubwa wa kituo”.

Akaongeza kuwa: “Hatukuishia kwenye swala la maji peke yake, bali tumefanya marekebisho ya mfumo wa umeme na ulinzi, kwa sasa yote inafanya kazi vizuri, wakazi wa kijiji hicho wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa msaada huu mkubwa wa kibinaadamu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: