Mahafali ya Quráni katika mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa miezi

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tawi la Bagdad chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya usomaji wa Quráni katika mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya na wasomaji wa Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya wameshiriki.

Tumeongea na mkuu wa tawi hilo Ustadh Nabiil Saaidiy amesema kuwa: Tunafanya hafla hii kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Maimamu waongofu (a.s), aidha ni sehemu ya ratiba ya tawi katika kuhuisha matukio tofauti ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Akaongeza kuwa: hafla hii imehudhuriwa na wasomi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na wasomaji wengine wa Quráni, na tahadhari zote za kujikinga na maambukizi zimezingatiwa.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu kupitia matawi yake tofauti ni sehemu muhimu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya na kinalenga kusambaza elimu ya Quráni, na kuchangia katika ujenzi wa jamii inayo fuata mafundisho ya Quráni tukufu katika sekta zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: