Kuanza shindano la (Almaaul-Muiin) la filamu fupi

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuanza kwa shindano la (Almaaul-Muiin) la filamu fupi, linalo elezea utukufu wa Imamu Mahadi (a.f), shindano hili linafanywa kufuatia kukaribia kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (a.f).

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo bibi Asmahani Ibrahim amesema: “Shindano linalenga kusambaza uwelewa kuhusu Imamu Mahadi (a.f) pamoja na kila kitu kinacho husu Imamu wa zama zetu Mahadi (a.f)”.

Akasema: masharti ya shindano hilo ni:

  • - Mada zitakazo shiriki zizungumzie mambo yanayo husu Imamu Mahadi (a.f) na zisizidi muda wa dakika moja na nusu (1:30).
  • - Mshiriki anaweza kufanya zaidi ya kazi moja.
  • - Kazi iwe imetengenezwa rasmi kwa ajili ya shindano hili na isiwe imesha wahi kushiriki kwenye shindano lingine au kutolewa mahala pengine popote”.

Akabainisha kuwa: “Kazi zitengenezwe kwa kiwango cha (HD) na zitumwe kwa njia ya mtandao, tutaendelea kupokea kazi hadi tarehe mosi mwezi wa nne mwaka huu, zawadi zitatolewa kwa kazi nzuri zitakazo kamilisha sifa zote tulizo taja awali”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: