Juhudi kubwa ya uboreshaji.. majalada bora yakisasa zaidi hapa Iraq

Maoni katika picha
Mitambo ya kutengeneza majalada ya (Hard cover) na (Soft cover) inayo milikiwa na Darul-Kafeel na usambazaji ni yakisasa zaidi hapa Iraq, majalada hayo yanaubora mkubwa, utengenezaji huu unatokana na uhitaji wa viwanda vya uchapishaji na kuondoa haja ya kuagiza nje ya taifa, pamoja na kuhakikisha sekta hiyo inaenda sawa na maendeleo ya dunia.

Mkuu wa daru Mhandisi Farasi Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kiwanda cha uzalishaji kinamitambo ya uchapaji kutoka Ujerumani katika shirika la (Kolbs) na (DA260) yenye uwezo wa kutengeneza majalada (2400) kwa kiwango cha jalada (40) kwa saa.

Akabainisha kuwa: “Unaweza kutumia mitambo hiyo kutengeneza katoni za aina zote na ukubwa tofauti, malighafi zote zinazo tumika ni rafiki kwa mazingira na zenye ubora wa hali ya juu”.

Akaendelea kusema: “Mitambo hiyo inatumika pia kutengeneza majalada ya (soft cover) ya vitabu na madaftari pamoja na machapisho mengine, upande wa uzalishaji pia kuna kifaa cha (BF512) kinacho tumika (kuandika vitabu – kupangilia milango ya kitabu – kuweka jalada na kusawazisha jalada) kifaa hicho kinauwezo mkubwa na kinafanya kazi kwa kasi ya mizunguko (30) kwa dakika, kinauwezo wa kuzalisha majalada (1800) kwa saa”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunaenda pamoja na maendeleo ya sekta ya uchapishaji, tunamikakati maalum chini ya utaratibu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuhakikisha tunakuwa na kila kifaa kitakacho tuwezesha kujitegemea katika sekta ya uchapishaji wa vitabu kwa faida ya waandishi na wasambazaji, kwa kutoa machapisho bora kwa bei nafuu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: