Kumbukumbu ya kifo cha Ali Akbaru mbele ya kaburi la Ammi yake Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Ali Akbaru (a.s), baada ya Adhuhuri ya leo mwezi (10 Shabani 1442h) sawa na tarehe (24 Machi 2021m), imefanywa hafla ya ufunguzi wa dirisha la malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu pamoja na naibu wake, pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo na baadhi ya watumishi.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi alikuwa ni mmoja wa wahudhiriaji wa hafla hiyo na ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Leo tumehudhuria ufunguzi wa dirisha tukufu, kama ilivyo kawaida katika siku kama hizi hufanywa hafla ya kufunguliwa kwa dirisha tukufu la kaburi la Abulfadhil Abbasi, hafla hii huenda sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa Ali bun Hussein (a.s) aliye zaliwa tarehe kama ya leo”.

Akaongeza kuwa: “Hafla imefanywa katika mazingira yaliyojaa unyenyekevu kwa mwenye malalo takatifu, na kwa kufuata maelekezo yote ya idara ya afya, ilifunguliwa kwa kusoma Quráni tukufu kisha ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa pamoja, baada ya hapo ikafanywa majlisi ya kuomboleza chini ya uhadhiri wa Mheshimiwa Shekh Abduswahibu Twaaiy kiongozi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, akazungumzia kifo cha Ali Akbaru (a.s) na yaliyo jiri katika vita ya Twafu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: