Kupandikiza mfupa kwenye paja

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limefaulu katika upasuaji wa kupandikiza mfupa kwa mgonjwa mwenye umri wa zaidi ya miaka ishirini.

Daktari bingwa wa mifupa katika hospitali hiyo amesema kuwa: “Jopo la madaktari wetu limefanikiwa kupandikiza mfupa kwa mgonjwa katika awamu ya pili”akaongeza kuwa: “Tumepandikiza mfupa kwa kutumia kifaa cha (Shishi mughlaq) kinacho muwezesha mgonjwa kutembea muda mfupi baada ya upasuaji”.

Akaendelea kusema: “Mgonjwa alikuwa amesha wahi kufanyiwa upasuaji katika hospitali nyingine akawekewa kifaa ambacho kimeharibika baada ya miaka miwili”.

Akasema kuwa: “Mgonjwa anauzito wa kilo (15)”, akasema: “Mgonjwa ameruhusiwa kuondoka hospitali siku (4) baada ya upasuaji akiwa na afya nzuri”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma kwa kutumia vifaa-tiba bora na vya kisasa zaidi, chini ya madaktari bingwa wa kitaifa na kimataifa jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa katika hospitali za kimaiafa duniani.

Kumbuka kuwa hospitali ya kimataifa Alkafeel hualika madaktari bingwa walio bobea katika maradhi tofauti kila baada ya muda fulani, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: