Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili kimekamilisha maandalizi ya ziara ya Shaábaniyya

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, kimekamilisha maandalizi ya kuwapokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Shaábaniyya, chini ya mazingira makali ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili kimekamilisha maandalizi ya kupokea mazuwaru wa ziara tukufu ya Shaábaniyya, kwa kuweka tayali idara zote za ulinzi na utoaji wa huduma, sambamba na kuandaa sehemu za kuswalia na usomaji wa dua”.

Akaongeza kuwa: “Tumeimarisha utekelezaji wa kanuni za afya, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutumia vitakasa mikono na barakoa, pamoja na kugawa barakoa katika milango inayo ingia kwenye eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na kuongoza matembezi ya mazuwaru katika siku za ziara”.

Akaendelea kusema: “Watumishi wetu watafanya kila wawezalo kutunza usafi katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na maeneo yanayo zunguka uwanja huo”.

Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, ni sawa na vitengo vingine, kinafanya juhudi kubwa ya kuhakikisha kinatoa huduma bora kwa mazuwaru wa Imamu Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara kubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: