Maqaam yake tukufu imepambwa kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwake

Maoni katika picha
Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imepambwa vizuri kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Rais wa kitengo cha Maqaam bwana Adnani Dhaifu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika hili ni tukio muhimu sana katika Maqaam hii, watumishi wetu kila mwaka huandaa mapambo mazuri tofauti na siku zingine za kawaida, katika tukio hili hushiriki pia watumishi wa idara zingine, huwekwa mapambo kuanzia kwenye kubba hadi kwenye njia zinazo elekea katika Maqaam hiyo, pamoja na ndani ya ukumbi wake na sehemu yeto inayo zunguka Maqaam”.

Akaongeza kuwa: “Mapambo hayo ni pamoja na vitambaa vilivyo andikwa maneno ya pongezi kwa ajili ya tukio hili, na hadithi za Maimamu watakatifu (a.s) zinazo thibitisha kuzaliwa kwake na kuongoza serikali ya uadilifu, hali kadhalika yamewekwa mapambo ya taa za kumetameta juu ya kubba na kuta pamoja na kwenye njia zinazo elekea katika Maqaam hiyo tukufu”.

Kumbuka kuwa Maqaam ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseini unapo ingia Karbala kwa upande wa kaskazini, katika eneo la Baabu-Salaamah kaskazini ya malalo ya Imamu Hussein (a.s) na ipo umbali wa mita (650) takriban, ni mazaru mashuhuri yenye kubba refu, Maqaam hii imepewa jina la Imamu Mahadi msubiriwa (a.f), inasemekana kuwa Imamu Hujjat Almahadi aliswali sehemu hiyo katika moja ya ziara zake kwa babu yake Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: