Idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini kwa wanawake, inayo fungamana na ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya shindano liitwalo (Jua nyuma ya mawingu) kwa wanawake tu.
Shindano hili linafanywa sambamba na kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu wa zama (a.f) likiwa na maswali ishirini kuhusu uhai wake.
Sharti la kushiriki kwenye shindano hili, mshiriki hatakiwi kuwa na umri chini ya miaka (18), shindano litafanyika kwa muda wa siku mbili.
Ili kushiriki kwenye shindano ingia kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/4qofUdPqH8NW4UuGA
Kumbuka kuwa lengo la shindano hili ni kuitambulisha historia ya Maimamu watakatifu (a.s) na kufanyia kazi maneno yao na vitendo vyao pamoja na kufuata mwenendo wao.