Barua (80) za Mahadi: Zimetumwa na kundi la watoto katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake

Maoni katika picha
Watoto (80) wameshiriki katika zowezi lililo andaliwa na Maahadi ya Quráni tukufu kitengo cha wanawake, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, linalo husu kuandika barua na kuzituma kwa Imamu wa zama katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, ili kuonyesha hisia zao kupitia barua hizo na kuingiza mapenzi ya Imamu wa zama (a.f) katika nyoyo za watoto hao.

Kiongozi wa Maahadi hiyo bibi Manaar Jaburi amesema kuwa: “Hakika zowezi hili linajenga ushirikiano wa watoto na linaongeza mapenzi yao kwa Imamu wa zama (a.f), pamoja na kuwajenga kulingana na umri wao na kuwafanya wawe na tabia njema sambamba na kuongeza Imani ya kumsubiri Imamu na kusoma dua ya faraj”.

Akaongeza kuwa: “Hali kadhalika zowezi hili linawaandaa watoto kumsubiri Imamu Mahadi (a.f), zowezi lilikuwa zuri sana kutokana na idadi kubwa ya barua zilizo tufikia ndani ya muda mfupi tu usiozidi siku tatu, Maahadi imeandaa kamati maalum ya kuchambua barua hizo na kuangalia zenye ujumbe mzuri ambapo waandishi wake watapewa zawadi, matokeo yatatangazwa hivi karibuni”.

Akamaliza kwa kusema: “Zowezi hili pia linahusu kuelekeza wazazi wawafundishe watoto wao uwepo wa Imamu wa zama (a.f) kuwa ni jambo la kweli, jambo hilo sio ngano za kale bali lazima tuliishi kwa lugha inayo endana na umri wao pamoja na kiwango chao cha uwelewa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: