Mkuu wa fani za kibobezi: Kinacho fanywa na shule za Al-Ameed kinastahiki pongezi

Maoni katika picha
Mkuu wa kitengo cha ubobezi katika idara ya malezi hapa Karbala Ustadh Jawaad Nasru-Llah, amepongeza kazi zinazo fanywa na shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa namna inavyo toa mitihani yake kwenye mazingira magumu ambayo taasisi za elimu zinapitia katika taifa hili, na namna ambayo watumishi wake wamefanikiwa kupambana katika mazingira hayo na kuweza kufikia malengo yao.

Ameyasema hayo alipo tembelea shule ya Nuurul-Abbasi (a.s) ya wasichana na wavulana za msingi na sekondari, ameshuhudia ufanywaji wa mitihani na maandalizi mengine. Sambamba na kazi kubwa inayo fanyika ya kutatua changamoto za walimu na wanafunzi wakati wa kufanya mitihani, mheshimiwa pia amekutana na viongozi wa shule kwa lengo la kutambua uwezo wa malezi na ufundishaji walio nao walimu wa shule za Al-Ameed.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: