Pamoja na tahadhari ya kujikinga na maambukizi: Shule za Al-Ameed zimemaliza mitihani yake

Maoni katika picha
Shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zimekamilisha mitihani ya msimu wa kwanza na mitihani ya nusu mwaka, katika mwaka huu wa masomo, chini ya tahadhari kali ya kujilinda na maambukizi, mitihani imefanywa katika mazingira salama kiafya, chini ya maelekezo ya wizara ya malezi na wizara ya afya.

Rais wa kitengo hicho Dokta Ahmadi Kaábi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya juhudu kubwa zilizo fanywa na watumishi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu pamoja na idara za shule za Al-Ameed, imesaidia kufanyika mitihani samala”.

Akaongeza kuwa: “Mitihani ya wanafunzi wa ngazi zote, awali, msingi na upili, wavulana na wasichana, imefanywa kwa utaratibu mzuri baada ya kuweka mpangilio mzuri ndani ya kumbi za mitihani, pamoja na kuchukua tahadhari zote zilizo elekezwa na idara ya afya ikiwa ni pamoja na kupuliza dawa kila siku”.

Akafafanua kuwa: “Shule za Al-Ameed zilidumisha mawasiliano na wanafunzi wake na zilikua zinatoa masomo kwa njia ya mtandao, sambamba na kuwawezesha kuelewa masomo kwa urahisi jamba ambalo limewawezesha kufanya mitihani hii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: